Chama cha ACT Wazalendo kimeshauri kuwa Miji ya Mwanza, Dodoma, Arusha na Dar es Salaam ifungwe watu wasiingie wala kutoka kwa muda wa siku 30 na kutaka kuwe na ‘lockdown’ inayowiana na mazingira ya Tanzania yaani yaweza kuwa partial.
“Watumishi wa Umma katika Mikoa husika wafanyie kazi majumbani mwao, Ofisi za Umma zibakize mtu mmoja kwa Idara na kwa zile kazi ambazo hazihusishi kukutana na watu na iwe kwa zamu, pendekezo hili pia lihusishe Mashirika yote ya Umma kwenye Mikoa” ACT Wazalendo