Mshambuliaji wa Inter Milan ya Italia Romelu Lukaku ameomba radhi kufuatia comment yake aliyoitoa wakati wa interview yake ya January kuhusiana na wachezaji wenzake.
Pamoja na kuripotiwa kuwa Inter Milani itamuadhibu, Lukaku ameomba radhi kufuatia kauli yake aliyoitoa January kuwa wachezaji 23 kati ya 25 wa Inter Milan wana dalilia za maambukizi ya virusi vya corona.
Lukakua alinukuliwa akisema hivi katika mahojiano yake kituo cha TV cha Ubelgiji cha VIER kupitia instagrama LIVE baada ya wachezaji wa timu yake kurejea wakitoka likizo ya December.
“Tulikuwa na wiki ya mapumziko mwezi December, tulirejea kazi na nakuapia kuwa wachezaji 23 kati ya 25 walikuwa wanaumwa, sikutanii”>>>Lukaku
”Kila mmoja wetu alikuwa anakohoa na homa (katika mechi vs Cagliari January 26), tulipokuwa tunafanya warm up nilihisi joto kuliko kawaida, sikuwa nimeugua homa kwa miaka sasa”>>>Lukaku