Mastaa wa Tottenham Hotspurs Serge Aurer raia wa Ivory Coast na Moussa Sissoko wanaweza kuingia matatizoni baada ya kubainika kuwa wamevunja sheria za nchi (England) kuhusiana na kukaa karantini.
England baada ya kusimamisha Ligi iliwataka wachezaji ikiwemo raia wa kawaida kujitenga na kukaa majumbani kwao ikiwa kama ni njia moja wapo ya kupunguza maambukizi ya virusi vya Corona.
Serge na Sissoko wawili hao wanadaiwa kuvunja sheria za karantini baada ya kuonekana wakifanya mazoezi pamoja tena bila kuzingatia social distance, video yao ya kufanya mazoezi pamoja ilipostiwa instagram katika ukurasa wa Serge Aurer kabla ya baadae kuamua kuitoa.
Baadae wawili hao walioamba radhi kwa kutoa statement ya pamoja “Tunatambua kiwa kama wachezaji professional tunao wajibu wa kuwa mfano wa kuigwa (Role Models) hususani katika wakati wa kipindi kama hiki ambacho kila mmoja anakabiliwa na changamoto, tunaomba radhi kwakutokuwa mfano sahihi”