Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia Elibariki Geofrey mkazi wa Chekereni wilayani Arumeru, kwa tuhuma za mauaji ya mke wake Ester Elibariki, baada ya kumpiga risasi mbili kifuani na shingoni, kisha na yeye kujijeruhi nayo shingoni, na sasa anatibiwa kwenye Hospitali ya Mount Meru.
Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Koka Moita, ambapo amesema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa Aprili 23, 2020, majira ya saa 6:25 usiku, ambapo taarifa za awali zinabainisha kuwa mauaji hayo ya kikatili yamesababishwa na wivu wa mapenzi.
“Tukio hilo limetokea eneo la Chekereni, wilayani Arumeru, Mama aitwaye Ester Elibariki aliuawa kwa kupigwa risasi mbili na mume wake Elibariki Geofrey” Kamanda Moita
“Mwili wa marehemu huyo upo katika Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya uchunguzi, uchunguzi unaendelea ili kubaini nini chanzo halisi cha tukio hilo, japo taarifa za awali zinaonesha kuwa ni wivu wa mapenzi” Kamanda Moita