Staa wa Juventus na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo atarejea Italia siku ya Jumanne baada ya club yake kutangaza kuwaita wachezaji wake wote wa kigeni wakiokuwa wamerejea makwao.
Ronaldo ni miongoni mwa mastaa wa Juventus waliokuwa wameondoka Italia na kurejea katika mataifa yao, hiyo ikiwa kama sehemu ya kukimbia maambukizi ya corona ambayo Italia yalikuwa makubwa.
Kwa sasa Juventus wanakaribia kuanza kufanya mazoezi kwa pamoja kama timu baada ya wimbi la ongezeko la virusi vya corona kupungua Italia, Ronaldo anarejea Italia lakini atakuwa ana siku 14 za kujitenga katantini kabla ya kuanza mazoezi na timu, hiyo ni baada ya waziri mkuu wa Italia kutangaza kuwa timu zinaweza kuanza mazoezi May 18 ila tarehe ya kuanza kwa Serie A bado haijatajwa.