Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ametangaza ongezeko la wagonjwa wa Corona 196 nchini huku Tanzania Bara ikiwa na Wagonjwa 174 na Zanzibar wagonjwa 22 ambao walitolewa taarifa na Waziri wa Afya Wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid na kufanya idadi ya wagonjwa wa Corona nchini kufikia 480.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo wakati akigawa magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge wa majimbo mbalimbali tukio lililofanyika leo katika ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo Mlimwa jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema jumla ya wagonjwa waliopona imeongezeka kutoka 48 hadi kufikia 197, huku Zanzibar waliopona wakiwa 36 na Tanzania bara 83. Pia Waziri Mkuu amesema kumekuwa na ongezeko la vifo vya watu sita (6) na kufanya kuwa na vifo vilivyotoka na Corona nchini kufikia 16.
Kati ya wenye maambukizi 297 waliobaki, 283 wanaendelea vizuri na tiba na kusubiri ufuatiliaji wa afya zao na wengine 14 wako chini ya uangalizi maalumu wa madaktari ambao wanahitaji oksjeni (Oxygen) ya kuwasaidia kupumua pamoja na wale wenye magonjwa mengine ambayo yamejitokeza kwenye wodi.
Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuwaondoa washukiwa waliokua karantini ambao walishatimiza siku 14 baada ya uchunguzi wa kiafya kuonekana hawana maambukizi na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Itazame hii video hapa ujionee mwanzo mwisho
KIM JONG UN AMEJIFICHA KUKWEPA CORONA, TRUMP ASEMA ANAJUA KILA KITU “NIMEZUIA VITA YA USA NA KOREA”