Kiungo wa zamani wa Arsenal na Chelsea anayecheza AS Monaco ya Ufaransa kwa sasa Cesc Fabregas amethibitisha kuwa mama wa bibi yake amepona corona akiwa na umri wa miaka 95.
Fabregas ametangaza taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa twitter ikiwa ni wiki chache zimepita toka bibi huyo augue corona, huku wengi wakipoteza matumaini kwa madai ugonjwa wa corona unashambulia zaidi wazee na watoto.
”Amepona virusi vya corona akiwa na umri wa miaka 95, jana vipimo vimerudi amepona, mama wa bibi yangu ni shujaa lakini isingekuwa pasipo msaada wa manesi na madoctor ambao wametoa maisha yao kila wakati” >>> Fabregas
Siku mbili zilizopita Fabregas alikubali makato ya asilimia 30 ya mshahara wake ili kuwezesha wafanyakazi wengine walipwe mishahara yao ambao nao walikuwa katika wimbi la kukatwa mshahara.