Wizara ya Afya Kenya imesema Madereva 8 wa Malori kutoka Tanzania ambao wamebainika kuwa na corona, (saba kwenye mpaka wa kuingilia Kenya wa Namanga na mmoja mpaka wa Isebania), wote wamerudishwa Tanzania, wagonjwa hao hawajahesabiwa kwenye idadi ya wagonjwa wapya Kenya.
Wizara hiyo imesema wagonjwa wapya 21 wa corona wameongezeka na kufanya idadi ya maambukizi kufikia 758 kutoka 737 Kenya >“tumepima sampuli 1486 ndani ya saa 24, wagonjwa wapya ni 22 ambapo Wanaume ni 14 na Wanawake 7, mgonjwa mwenye umri mdogo ana miaka 7, mkubwa miaka 79”
Wizara hiyo ya Afya Kenya imesema licha ya maambukizi kufikia 758 nchini humo lakini wameendelea kupambana na kuhakikisha wagonjwa wanapona ambapo hadi sasa wamepona wagonjwa 284, ila wagonjwa wawili wengine wamefariki Dunia na kufanya vifo vya corona nchini humo kufikia 42 kutoka 40.
LIVE MAGAZETI: Mbowe, Polisi kimenuka tena, Mwongozo wa kuzika waliokufa kwa corona waja