Wabunge wote wa CHADEMA ambao wanahitimisha siku 14 za kujitenga kwa kukaa nyumbani na kutohudhuria shughuli za Bunge, vikiwemo vikao vya Bunge, ndani ya ukumbi na kamati zake, leo Ijumaa wanatarajiwa kurejea Bungeni baada ya kuwa na uhakika kuwa hawana corona.
…>>>>“Wabunge wetu wote waliotekeleza makubaliano na uamuzi wa Chama na Wabunge wa kujitenga kwa siku 14 ambayo yanatokana na maelekezo na ushauri wa Wataalamu wa afya ikiwemo WHO, leo watarejea Bungeni kuendelea na majukumu yao, huku wakiendelea kuchukua tahadhari”– John Mnyika, Katibu Mkuu CHADEMA
VIDEO: Mke wa Mengi Kafunguka na kukabidhi msaada kwa Walemavu kuepuka Corona