Juma Duni Haji akiwasilisha maoni ya wachache kutoka kwenye kamati namba 11 ambapo alianza kwa kusema >>> ‘hoja za wengi ni muundo serikali ya shirikisho kuua udugu, kwani kabla ya muungano hatukua na udugu’
Kuna wajumbe wanasema kuirudisha serikali ya Tanganyika ni kufufua makaburi, kwani imezikwa? ninachofahamu mimi Tanganyika imekufa kwa kubadilisha jina tu.
Wengine eti serikali3 zitarudisha usultani Zanzibar, Loooooh! Mashaaalah, baada ya miaka 50 tunayazungumza haya? katiba ya sasa kifungu 98b kimetoa ruhusa Watanganyika na Wazanzibar wakikubaliana muungano utavunjika sio lazima serikali 3.
Mabunge ya sasa yana wajumbe wasiopungua 438 ya serikali 3 yatakua na 314 sasa mtu anaibuka tu na kusema serikali 3 gharama.
Ikaelezwa Zanzibar kuruhusiwa kutafuta misaada nje kwa nini mliizuia sasa baada ya serikali 3 mmerejesha? ikaelezwa pia mafuta kuondolewa ktk orodha ya mambo ya muungano, ni miaka7 hii lilipitishwa, kisa serikali 3 ndio mnaliondoa?
Katika dharau tunayofanyiwa kwa udogo wetu Znz tunaambiwa hatuna uwezo kuchangia muungano, pato la Mznz na Mtanganyika halina tofauti, Tanganyika ni kubwa lakini kwa mmojammoja umasikini wetu ni sawasawa
Makusanyo ya muungano yanayotumika kwa muungano hayajazidi 35% ambapo si chini ya 60% yaliyobaki yanatumika Tanganyika, hizi tume ambazo haziundwi na account kutofunguliwa ni kwa sababu mapato haya Znz haitakiwi kupata.
Sifa ya Zanzibar kwa miaka 50 kama serikali hizi mbili kweli zilikua na nia njema, Zanzibar ingekua sasa Hongkong ya Afrika.
Znz haina benki kuu wala sarafu yake na sera zote za uchumi ziko chini ya Muungano, Zanzibar mmeifunga miguu na mikono, leo kutatua matatizo ya Muungano kwa mfumo wa serikali 3 linatangulizwa swala la gharama, kwani lini zilikua ndogo?
Nilisoma kwenye magazeti miaka 50 uhuru wa Tanganyika si chini ya Bilioni 70 zimetumika katika sherehe, sherehe zenyewe za uwanja wa taifa kutazama gwaride watu wanavyorusha viatu, hayo hayo miaka yote.
Mikoa ya Tanganyika wakati wa 64 ilikua 17 tu ila sasa haipungui 26, Wilaya zilikua 60 mpaka 70 lakini sasa hazipungui 150, kila ukipanua madudu haya unaongeza gharama za utawala, yanatuhusu nini sisi Wazanzibari magharama haya?
Alichofanya Warioba ni kujaribu kusahihisha haya ya miaka 50, baada ya kutusaidia wengi mnataka hali hii iendelee?
Hayo ndio yaliyowasilishwa na Juma Duni Haji, ya Ummy Mwalimu yanafata muda sio mrefu… ila unaweza kuacha maoni yako hapa chini kuhusu haya ya Juma Haji.