Zoezi la urejeshwaji wa mawasiliano ya njia ya reli kati ya Tabora na Katavi umekamilika na treni za mzigo kuanza kupita ambapo msimamizi wa matengenezo hayo kutoka Shirika la Reli nchini Mhandisi Machibya Masanja kuwataka Watanzania na Viongozi kuwaamini Wahandisi wa ndani.
Akitoa pongezi na shukrani baada ya zoezi hilo lililotumia siku 23 kuunganisha kipande cha zaidi ya mita 120 kilichosombwa na maji katika eneo la mto Ugala Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama ameomba Taasis zingine zinazosimamia ujenzi wa miundombinu kutumia Wahandisi hao katika maeneo yaliyokata mawasiliano kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuharibu miundombinu.