Shirika la Afya duniani lilisema itabidi Watu wajifunze kuishi na corona maana haionekani kama itaisha leo, sasa katika kuishi nayo mambo inabidi yaendelee zikiwemo Shule, Shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo safari za Ndege.
Kampuni ya Uingereza RAS inayojishughulisha na utengenezaji wa vifaa vya ndani ya Ndege imekuja na wazo la kutengeneza kifaa mithili ya kioo kitakachowekwa katikati ya kiti na kiti ili kujikinga na corona kati ya abiria na abiria.
Kampuni hiyo imesema kwa sasa inasubiria tu kibali kutoka Mamlaka ya anga ya Umoja wa Ulaya ili abiria waanze kuuziwa kifaa hicho wiki chache zijazo ambapo kampuni hiyo imelenga zaidi kutenegenza size za kuweka kwenye daraja la economy kwenye ndege sababu sehemu hiyo ndio viti vya abiria huwa vimesogeleana sana.