Juni 13 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Uelewa kuhusu Ualbino (IAAD) ambapo maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika kupitia vyombo vya habari kutokana na janga la ugonjwa wa Covid-19.
Shirika la ‘Under The Same Sun’ (UTSS) linaloshughulika na haki za watu wenye Ualbino linaadhimisha siku hii kupitia vyombo vya habari.
Kihistoria Siku ya Kimataifa ya Uelewa kuhusu Ualbino (IAAD) ilitangazwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mwaka 2014 na kwa hiyo inaadhimishwa ulimwenguni kote.
Watu wenye Ualbino wanakabiliwa na aina nyingi za ubaguzi ulimwenguni kwa sababu hali hiyo haifahamiki vizuri kijamii na kimtazamo.