Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti ametoa onyo kali kwa watu wanaodhani kila anayetoa misaada anataka kugombea nafasi za Uongozi .
Mnyeti amesema hayo wakati akipokea msaada wa vifaa vya kujikinga na Corona ikiwemo vitakasa mikono, sabuni, pamoja na vyakula kwa makundi ya watoto na wazee wasiojiweza.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brand David Mulokozi ameipongeza serikali kwa juhudi za kukabiliana na ugonjwa corona kwani vifaa hivyo vitaongeza nguvu katika mapambano dhidi ya corona.
Mwakilishi wa Makundi yaliyopokea msaada huo Samson Munuo amepongeza wadau hao kwa kujitoa kusaidia jamii hususan makundi yaliyosahaulika