Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amekwenda kutoa pole kwa familia ya Balozi Mstaafu Job Lusinde aliyefariki dunia July 7, 2020.
Msiba wa Balozi Mstaafu Lusinde upo nyumbani kwake Kilimani Jijini Dodoma.
Akiwa nyumbani kwa Marehemu Balozi Mstaafu Lusinde, Rais Magufuli amekutana na Mjane wa Marehemu Sara Lusinde, ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu ambapo ameeleza kuwa kuguswa na kifo cha Balozi Mstaafu Lusinde na kwamba daima atamkumbuka kwa mchango wake alioutoa akiwa Waziri wa Ujenzi, ushauri wake mzuri na moyo wake wa upendo na ukweli.