Club ya Aston Villa ya England inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta leo ilicheza mchezo wake wa mwisho wa Ligi Kuu England 2019/20 katika uwanja wao wa Villa Park dhidi ya Arsenal, mchezo huo ulikuwa ni mchezo muhimu kwa Aston Villa wanaopambana kutoshuka daraja.
Aston Villa wakiwa nyumbani wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lilifungwa dakika ya 27 na Trezeguet katika mchezo ambao Mbwana Samatta alicheza kwa dakika 72 za mwanzo, ushindi huo umeifanya Aston Villa kufufua matumaini ya kusalia Ligi Kuu kwa msimu wa 2020/21 kwani wamesogea hadi nafasi ya 17 wakiwa na point 34.
Hivyo kufuatia ushindi huo sasa Aston Villa watahitaji ushindi katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya West Ham United wenye point 37 pia ambao July 22 watacheza dhidi ya Man United lakini kubwa kwa Aston Villa hatma yao kubaki au kushuka wataamua wenyewe July 26 2020 dhidi ya West Ham United wakiwa ugenini kwani watahitaji ushindi huku wakimuombea Watford apoteze katika mchezo wake dhidi ya Arsenal.
Mchezo wa leo Aston Villa walifanikiwa kuidhibiti Arsenal kwa kiasi kikubwa na kuifanya ishindwe kupiga shuti hata moja lililolenda lao, hiyo ikiwa ni mara ya pili kwa Arsenal kumaliza mchezo bila kupiga shuti hata moja lililolenga lango msimu huu baada ya hali kama hiyo kutokea katika mchezo wao dhidi ya Man City.
VIDEO: KIMENUKA YANGA, MORISSON KASUSA AKIMBIA NJE UWANJANI “ACHA MASHABIKI WANIPIGE”