Ubalozi wa Amerika katika mji wa China wa Chengdu umefungwa baada ya muda uliotolewa wa masaa 72 kumalizika. China iliamuru kufungwa kwake kufuatia Amerika kufunga ubalozi wa China huko Houston, Texas, wiki iliyopita.
Kabla ya tarehe ya mwisho ya Jumatatu ya leo, wafanyikazi wa ubalozi huo walionekana wakiondoka katika jengo hilo, jalada limeondolewa, na bendera ya Amerika tayari imeshushwa. Wizara ya mambo ya nje ya China imesema wafanyikazi wa China waliingia kwenye jumba hilo la ubalozi wa Amerika baada ya tarehe ya mwisho na “kuchukua madaraka”.
Marekani imesema imesikitishwa na uamzi huo wa china kwasababu ubalozi huo ndio umekuwa kama kitovu cha uhusiano na Uchina Magharibi kwa miaka 35.