Watu wenye silaha nzito wamevamia gereza lililoko Mashariki mwa Jiji la Afghan, Jalalabad na kuzua mapigano makali dhidi ya walinzi wa gereza hilo.
Kwa mujibu wa Aljazeera, watu kadhaa weamejeruhiwa katika mapigano hayo, huku vyombo vya ulinzi vikiendelea kuongeza nguvu katika eneo hilo.
Sohrab Qaderi, ambaye ni mmoja kati ya maafisa usalama wa Jalalabad, amesema kuwa washambuliaji walikuwa wamejihami na gari lenye vilipuzi nje ya jengo la serikali.
“Takribani watu 20 wamejeruhiwa, na mapigano yanaendelea hivi sasa,” Qaderi amenukuliwa na Aljazeera
Chombo cha habari cha Afghan, TOLOnews kimemkariri shuhuda mmoja akieleza kuwa mtu mmoja amefariki katika mapigano hayo, lakini vyanzo vyenye mamlaka bado havijathibitisha ukweli wa taarifa hiyo.
Kundi la Talban limekana kuhusika na tukio hilo. Msemaji wa kundi hilo ametumia mtandao wa Twitter kueleza kuwa hawahusiki kwa namna yoyote na shambulizi hilo lililoibuka siku chache baada ya kuingia makubaliano na Serikali kusitisha mapigano.
Shambulizi hilo limekuja baada ya wakala wa kijasusi wa Afghan kuripoti kuwa makomando wa nchi hiyo walimuua kamanda mwandamizi wa kundi la kigaidi la ISIL karibu na Jalalabad.
BALOZI WA MAREKANI AVUA BARAKOA MBELE YA RAIS MAGUFULI, MAGUFULI AMPONGEZA AANGUA KICHEKO