Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe kusitisha utoaji leseni mpya ya uchimbaji wa makaa ya mawe kwa kampuni ya TANCOUL ENERGY LIMITED na ameagiza timu maalum kuchunguza mikataba iliyowekwa kati ya kampuni ya TANCOUL ENERGY LIMITED na Serikali kupitia taasisi ya NDC.
Bashungwa ametoa maagizo hayo August 3, 2020 alipotembelea na kukagua mradi wa uchimbaji wa makaa ya mawe katika mgodi wa Ngaka uliopo eneo la Ruanda wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma.
“Makaa ya mawe bora yabaki ardhini kuliko kuchibwa lakini serikali hainufaiki na Chochote, ili tukipata wabia wazuri ambao wapo tayari kutoa sitahiki za nchi kulingana na mikataba iliyowekwa ili mwekezaji wapate asilimia zake pia sisi kama serikali tupate sehemu yetu” Bashungwa.
“Tume maalum iliyoundwa kwa kushirikiana na Katibu Mkuu, chukueni mkataba wa Tancoul uwekeni kwenye mzani kwa kutumia sheria ili kama kuna mikataba mibovu haitufai, tuanze upya na hisa ambazo tunasitahili kuzipata, tuzipate maana hatumezi kuwa na taasisi ya NDC yenye rasilimali nyingi lakini ni masikini ya kutupa” Bashungwa