Usiku wa April 13 2014 kwenye baa iitwayo ‘Arusha night park’ iliyopo Mianzini Arusha ambayo siku zote ni miongoni mwa sehemu zinazokua na mkusanyiko wa watu wengi kuanzia jioni, limerushwa bomu katikati ya watu mbalimbali wakitazama mpira.
millardayo.com ilipata nafasi ya kuongea na mkuu wa mkoa wa Arusha usiku huohuo ambae ni kiongozi wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ambae amethibitisha kwamba ni watu 15 wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.
Anasema wote wamepelekwa hospitali ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha bomu hilo ni la kutengenezwa kwa mkono na mpaka sasa hajajulikana alietekeleza shambulio hilo ambalo hata hivyo halikugharimu maisha ya yeyote.
Wengi walioumia ni wahudumu wa baa hiyo ambapo wengine walikatika miguu na mikono ambapo wamepokelewa kwenye hospitali tatu tofauti Arusha mjini za Mount Meru, Seliani na St. Elizabeth.
Kama unahitaji kila ninachopata kikufikie, jiunge na familia ya millardayo.com kupitia twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo la MillardAyo.