Mama Rahel Joashi mwenye umri wa miaka 56 Mkazi wa Musoma mkoani Mara anayetumia usafiri wa baiskeli kusambaza vinywaji aina ya bia kwa muda miaka 20 kwa ujira wa shilingi mia mbili amefanikiwa kusomesha watoto wake wanne mpaka elimu ya Chuo Kikuu na mmoja kuajiriwa.
Akipiga story na AyoTV Mama huyo ameeleza kuwa ugumu wa maisha ulichangia kumpa fursa na kutumia baiskeli kama mtaji, ambapo Mumewe alimwacha akahamia Kijijini na kumtaka aachane na kazi hiyo inayomdhalilisha mwanamke.
Joashi ameeleza kuwa awali alikuwa anagombana na Mume wake juu ya utoaji wa hela ya matumizi nyumbani pale Mume wake asemapo hana hela lakini kwa sasa anajionea mwenyewe kuhusu kutoa huduma ya matumizi nyumbani.