Baada ya kutekwa nyara kwa muda wa miaka 3 wakenya wawili waliokua wakihudumia kwenye shirika moja la Kijamii la kutoa misaada wameachiwa huru,Wakenya hao ni James Gishoi mwenye miaka 53 na Daniel Wanyoike 25 ambao wamekutana na jamaa na marafiki baada ya kusafirishwa kwa ndege hadi Nairobi kutoka liboi.
Madereva hao wawili wa shirika la Care International walitekwa nyara na kuzuiliwa katika Magereza yanayo shikiliwa na wapiganaji hao ambapo Ilimbidi Daniel wanyoike ajisalimishe ili kuachiliwa kwa wapiganaji hao.
Wawili hao wamesema kwamba uadui kati ya Al Shabaab na Raia wa Kenya ulichochewa na hatua ya Kenya kuwapeleka maafisa wake wa jeshi nchini humo James na Daniel wamesema kwamba wameshuhudia mateka wenzao wakichinjwa na kupigwa risasi mbele yao kwa miaka yote mitatu Ambayo wamekua katika gereza la Barahwe ingawa wamekua wakiamishwa kila wakati.
Aidha mateka hao walitembea kilomita 40 magharibi mwa jiji la Barahwe kuelekea mji wa Dobley ili kukutana na jeshi la Amisom,wakuu wa jeshi la Kenya KDF wamesema kwamba wataendelea kuwashikilia wawili hao huku wakipewa ushauri nasaha na kuwahoji ilikupata taarifa zaidi kuhusu wakenya na Raiya wa nchi zinginezo walio salia kwenye mikono ya wapiganaji wa al shabaab.