Harusi ya Ephrahim Jonasi ambaye ni mtumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA) na Bisunga Nyabusani imelazimika kuahirishwa baada ya Mhasibu kutokomea na baadhi ya fedha za michango.
AyoTV na millardayo.com ilifika katika ukumbi wa Niteshi uliopo Mjini Kahama Majira ya saa 2:00 usiku Agosti 16,2020 ili kujua kwa undani wa tukio hilo baada ya kupata taarifa za sherehe hiyo kuahirihwa kimya kimya na kuzua taharuki kwa wageni waliochangia michango ya harusi hiyo.
Mmoja ya wageni waalikwa, Marco Jakson aliyefika katika ukumbi huo saa moja kamili usiku alisema kuwa yeye hakuwa na taarifa zozote za kuahirishwa kwa sherehe ya harusi hiyo kwani jana yake alipewa kadi ya mwaliko na waandaji ikimtaka kufika katika Ukumbi wa Niteshi kuanzia saa 12:00.
“Nimekaa hapa kwa muda wa masaa matatu lakini naona watu wanakuja na kuondoka hapa ukumbini ukiwauliza wanasema sherehe imeahirishwa sasa kama imeahirishwa viongozi wa sherehe hii wako wapi na kwanini wasije ukumbini kuwaomba watu radhi na kutuambia kunashida gani,” Marco