Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keïta amejiuzulu muda mfupi baada ya kuwekwa kizuizini na Jeshi la nchi hiyo.
Akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni, Bwana Keïta amesema anaivunja serikali na bunge.
”Sitaki damu imwagike ili mimi kuendelea kubaki madarakani,” Kaita
Hatua hii imekuja saa kadhaa baada ya kiongozi huyo wa juu na Waziri Mkuu Boubou Cissé kupelekwa kwenye kambi ya jeshi karibu na mji mkuu Bamako, hatua iliyosababisha mataifa ya Afrika Magharibi na Ufaransa kulaani kitendo hicho.
”Ikiwa leo, sehemu ya vikosi vilivyo na silaha wanataka hili liishe kwa kuingilia kati, nina cha kufanya?’‘ Keïta.
Rais huyo pamoja na waziri mkuu wake walikamwatwa na jeshi baada ya maandamano yaliyodumu kwa miezi kadhaa kumtaka bwana Keita kung’atuka madarakani.
Keita ambaye alikua katika muhula wake wa pili wa uongozi alikua akituhumiwa kusababisha mdororo wa kiuchumi nchini humo pamoja na kushindwa kuyazuia makundi ya wapiganaji wa kiislamu ambayo yameharibu amani ya nchi hiyo.