Watu watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka saba, yakiwemo ya kushiriki vikao vya kutengeneza mikakati ya ugaidi, kukutwa na vilipuzi, silaha na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania( JWTZ).
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao, leo Agosti 19, 2020 na Jopo la Mawakili watatu wa upande wa mashtaka, wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Shadrak Kimaro akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon na Tulimanywa Majigo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Washtakiwa wao ni Halifa Hassan, Adam Kasekwa, maarufu kama Adamo na Mohamed Lingwenya, ambapo kwa pamoja wamesomewa kesi ya uhujumu uchumu namba 63/2020 chini ya sheria ya usalama wa taifa na sheria ya kuzuia makosa ya ugaidi.