Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa hii leo amesaini sheria inayozuia wanafunzi wa kike nchini humo kukatishwa masomo yao pindi wanapopata ujauzito.
Hatua hii imekuja baada ya uwepo wa ugumu kwa wasichana nchini humo, kuendelea na masomo wanapopata ujauzito lakini sheria hii itaenda kuwalinda.
Tangu kuibuka kwa janga la ugonjwa wa Virusi vya Corona, nchi nyingi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara limeshuhudia idadi kubwa ya watoto wa kike wakipata ujauzito kipindi cha likizo.
Hali hii huenda ingekuwa tishio kwa wasichana wengi nchini Zimbabwe kukosa masomo yao kabla ya kuidhinishwa kwa sheria hii ambayo inakomesha matumizi ya bakora kwa lengo la kuwaadhibu wasichana wajawazito wawapo shuleni.
Sheria hii imekuwa na uungwaji mkono wa watu wengi wakidai, inatoa nafasi sawa kwa wanafunzi wa kike na wa kiume kuweza kumaliza masomo na kutimiza ndoto zao pasi na vikwazo vyovyote vya unyanyasaji wa kijinsia.
USIPITWE NA HII >>> JINAMIZI LINALOKABA USIKU, NI HATARI LINAUA