Mtanzania yeyote ambae anajua utaratibu wa usafirishaji kwenye nchi zilizoendelea kama South Africa, Uingereza na mataifa mengine duniani, anaweza kushawishika kutamani utaratibu huo ungekua unapatikana pia na nyumbani Tanzania.
Nilikua natazama TBC1 nikaona interview fupi ya Waziri wa uchukuzi Harrison Mwakyembe na nikafanikiwa kuipata akisema itajengwa reli mpya nchini Tanzania kwa nguvu ya benki kuu ya Uingereza baada ya kuona umuhimu wa matumizi ya reli kusafirisha mizigo na abiria ili kuepukana na yote yanayotokea barabarani.
Taarifa ilisema pia kuna mpango wa baadae wa kuleta treni za kisasa zinazotumia umeme ambazo zina sifa ya kufanya kazi kwa uharaka na uhakika kote duniani.
Una chochote cha kusema kuhusu hili?
Kazi ya millardayo.com ni kuhakikisha kila taarifa muhimu inakufikia wakati wowote ambapo kama unashinda sana kwenye mitandao ya kijamii, nitakua nakutumia kila stori ukijiunga na mimi twitter, instagram na facebook kwa jina hilohilo la millardayo.com