IGP Mstaafu Balozi Ernest Mangu amesema kuwa amehitimisha safari yake katika utumishi wa Jeshi la Polisi Tanzania akiwa salama na ameliacha Jeshi hilo likiwa na mafanikio.
IGP mstaafu Mangu amesema hayo katika hafla ya kuagwa iliyofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Kurasini jijini DSM, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Christopher Kadio.
“Hakuna changamoto iliyoniteteresha katika uongozi wangu, ila kuna matukio makubwa ambayo hatukuyatarajia yalitokea katika Uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo Mawaziri Wakuu Wastaafu wawili walihamia upinzani walisababisha mtikisiko kidogo ila tulimaliza salama” Mangu