Mwaka 1997 Marina Granovskai alikuwa msaidizi Binafsi wa Bilionea wa Chelsea Roman Abromavich katika kampuni ya mafuta (Sibneft) na baadae 2003 baada ya Chelsea kununuliwa na Roman Abromavich, Bi Marina akaanza kufanya nayo kazi taratibu hadi 2014 akatangazwa rasmi kuwa Mkurugenzi wa Chesea.
Toka Mwaka 2016 Barbara Gonzalez alikuwa msaidizi wa Rais wa makampuni ya MeTL Group Mo Dewji ambaye baadae aliwania zabuni za kununua hisa za Simba SC asilimia 49 na kufanikiwa, Barbara akiwa anashirikiana nae katika mfumo wa mabadiliko, baadae mjumbe wa Bodi na alipoondoka CEO Senzo Mbatha raia wa Afrika Kusini Barbara akakaimu nafasi ya U-CEO Simba SC na September 5 2020 Bodi ya Wakurugenzi Simba wakamtangaza kuwa CEO kamili
Kwa mujibu wa jarida la Forbes 2018 akatajwa kuwa Mwanamke namba 5 mwenye nguvu katika michezo ya kimataifa, Chelsea ndio ilikuwa club yake ya kwanza Marina kuwahi kuifanyia kazi kama ilivyo kwa Barbara na Simba SC.