Katika maadhimisho ya siku ya wahanga wa majeraha ya uti wa Mgongo duniani (World Spinal cord Injury day) asasi za The Mariam Spinal Cord Injuries foundation na Dkt. Reginald Mengi foundation na nyingine zimetoa zawadi kwa wagonjwa wenye jeraha la uti wa mgongo wanaotibiwa hapa MOI.
“Serikali hii sikivu ya awamu ya Tano imetuwezesha kuwa na vifaa vya uchunguzi vya kisasa vya XRay za kidijitali, CT Scan na MRI, tuna vyumba vya upasuaji 9 vya kisasa, tunao wataalamu wabobezi ambao wanawapa huduma wogonjwa kwa weledi” Respicious Boniface Mkurugenzi Mtendaji MOI
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mariam Kassim Oberet amesema “Nimeanzisha hii Asasi ili kuwasaidia wenzangu walio na matatizo ya Uti wa mgogongo, Mimi mwenyewe nina matatizo ya uti wa mgongo”.
“Nimeanzisha baada ya kuona watu wenye matatizo haya wanateseka, wengine wanatengwa wanakosa vifaa vya kuwafanya kufika Hospital kupatiwa matibabu ikiwemo wheel chair” Mariam
“Kiukweli tumekuwa tunatengwa na jamii, Mimi nilipopata ajali mahusiano yangu yaliharibika niliachika, wasitutenge” Mariam