Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za wizi baada ya kuvunja Mahakama ya Wilaya ya Njombe na kuiba vitu mbalimbali vya ofisi hiyo ikiwemo Laptop tatu (3) na Sukari kiasi cha Kg 25, waliokamatwa yupo aliyeiba na mwingine aliyeenda kuuziwa Laptop hizo.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah na kuongeza kuwa tukio hilo ni la ajabu na hivyo wanangoja utaratibu ukamilike tu ili waweze kuwafikisha mahakamani kwa kuiibia Mahakama.
“Huwezi ukaamini na ninaomba uamini, kuna watu wameenda wamevunja Mahakama ya Wilaya ya Njombe, hivi ninavyoongea hapa Mahakama hiyo ilivunjwa, ikaibiwa vitu mbalimbali ikiwemo sukari Kg 25, na laptop 3, tumeweza kukamata hizo laptop na watu wawili tumewakamata, yaani watu walivyo majasiri hawaogopi hata vyombo ambavyo vinawatendea haki” Kamanda Issah
ESTER BULAYA AWAKA “MSINIFANYE MTOTO MNA-COPY HADI MAKOSA MTU ASIYE NA MVUTO SIYO SAIZI YANGU”