Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo, Bernard Membe amesema wakati anaondoka CCM na kukaa kama raia wa kawaida mpaka alipojiunga na chama hicho alijisikia kuwa na raha sana kulinganisha na kule alikokuwa.
Membe “Ndani ya ACT-Wazalendo kuna vijana wenye akili hajapata kuona na wanajadili, kukosoa na kukosoana chini ya Uongozi wa Maalim Seif na baadae wanatoka wakiwa kama timu”
Membe mesema, akijilinganisha na wagombea wengine anajiona kuwa ni mtu anayefaa zaidi kutokana na uzoefu mkubwa alio nao katika uongozi wa ndani ya nchi na nje ya nchi na ingekuwa dhambi kubwa sana kama asingegombea nafasi ya Urais.
Aidha, ameongeza kuwa fedha za kununua ndege na kujenga reli hazijatoka kwa Watanzania bali kwenye mabenki ya nje na uwekezaji huu hauleti faida ya haraka kwa ajili ya kulipa hayo madeni, Hakuna Serikali Duniani inayomiliki ndege, bali ni biashara za watu na Serikali huweza tu kuchukua hisa.