Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa mwezi Oktoba, Novemba na Desemba ambapo maeneo mengi ya Nchi yanatarajiwa kupata mvua chache jambo linaloweza kuleta athari ikiwemo upungufu wa chakula.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Rais wa WMO Dkt. Agnes Kijazi aliwataka wananchi wa maeneo hayo kuzitumia vizuri mvua hizo kwa kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa sekta husika kwa vile maeneo mengi yanatarajiwa kuwa na mvua za kutosha.
“Naendelea kutoa rai kwa wananchi wa mikoa husika kuzitumia mvua hizi kwa kupanda mazao sahihi kwa kufuata ushauri wa wataalamu, kama tunavyoona maeneo mengi yatarajiwa kuwa na mvua za juu ya wastani hadi wastani” Dkt. Kijazi
Aidha, Dkt. Kijazi alifafanua kuhusu mvua zinazoendelea kunyesha kwa maeneo ya Kaskazini mwa nchi kwa kusema kuwa mvua hizi ni za msimu wa vuli kwa maeneo yanayopata mvua mbili kwa mwaka na katika kipindi hiki cha vuli kunatarajiwa kuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa ambapo alimalizia kwa kuwataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na TMA sambamba na kuchukua tahadhari ya vipindi vifupi vya mvua kubwa,upepo mkali na mawimbi makubwa, vinavyotarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo.
Utabiri uliotolewa kwa maeneo yanayopata mvua za msimu mara moja kwa mwaka unaonesha maeneo ya mengi ya mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Songwe, Ruvuma, Njombe, Iringa, Rukwa Kusini mwa mkoa wa Morogoro, Lindi na Mtwara, yanatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani hadi wastani na maeneo ya mikoa ya Kigoma na Katavi, yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.
MWANRI AIBUKA AMVUNJA MBAVU WAZIRI MKUU ABAKI HOI KWA KICHEKO, WIMBO MBEGE IKIISHA KIBORORILONI