Leo September 9, 2020 Moto mkubwa umetokea msituni katika Jimbo la California nchini Marekani na kuteketeza Ekari zaidi ya 135,000 pamoja na kuharibu miundombinu zaidi ya 65 ikiwemo makazi ya Watu.
Moto huo unadaiwa kusabaishwa na wanandoa ambao walikuwa wakifanya sherehe ya kujua jinsia ya mtoto aliyeko tumboni kwa mama (Gender reveal party).
Shughuli za kuokoa watu bado zinaendelea huku jitihada mbalimbali zikitumika kuweza kuudhibiti moto huo.