Leo September 11, 2020 Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo na kuachiwa kwa dhamana.
Kubenea alikamatwa Septemba 07, 2020 na kutuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuingiza fedha za kigeni bila kutoa tamko na kuingia Nchini kinyume cha Sheria ya Uhamiaji.
Baada ya kukamatwa alifikishwa Mahakamani na kisha kurudishwa rumande kutokana na makosa ya utakatishaji fedha kutokuwa na dhamana.