Leo September 13, 2020 Mgombea Ubunge wa tiketi ya CCM, Jimbo la Vunjo, Moshi Vijini, Dkt .Charles Kimei amewaomba wananchi wa Jimbo hilo kumpa ridhaa ya kuwa Mbunge wao ili aweze kuwaletea mapinduzi ya kiuchumi.
Ameyasema hayo katika Mkutano wa uzinduzi wa kampeni zake uliofanyika katika Mji mdogo ya Himo na kuratibiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Jimbo hilo.
Katika hotuba yake, Dkt. Kimei amesema kuwa Jimbo hilo lina changamoto nyingi ikiwamo miundombinu mibovu ya barabara, elimu, afya na ukosefu wa masoko thabiti kwa mazao yazalishwayo na wakazi wa jimbo hilo.
“Kwa kushirikiana na wadau wengine, tunakamilsha mchakato wa kuanzisha mfuko wa Wajasiliamari Vunjo. Mimi mwenyewe nitatoa andiko la mradi yaani (Project write-up) ili kupata fedha za uwezeshaji wa makundi maalum ya Wakulima, Wafugaji, Vijana, Wanawake, Bodaboda na mafundi makenika kwa kuwapa mikopo nafuu” Kimei
”Jambo kubwa la msingi ni kuanzisha viwanda vya usindikaji ili kuongeza thamani ya mazao yetu. Badala ya kuuza Mpunga, tutaanza kuuza mchele wetu uliofungwa vizuri, badala ya kuuza nyanya ambazo huharibika kirahisi, viwanda hivi vitasindika nyanya hizo na tutauza tomato paste yetu wenyewe hivyo kuongeza thamani na vipato vya wananchi wa Himo, tutafanya hivyo pia kwa mazao ya Kahawa na mengineyo’ Kimei
“Tutasimamia kukamilisha ujenzi wa hospitali wa Wilaya ya Himo ambao ulisimama, pia tutashughulikia masuala ya Bima za afya na matibabu kwa Wazee, kuhusu ukosefu wa gari la Wagonjwa, Kimei amesema kwa sasa, Jimbo letu halina gari la uhakika la kubebea wagonjwa, naahidi kutoa gari langu mimi mwenyewe, lifanye kazi hiyo wakati tunaendelea na mchakato wa kuongeza mengine” Kimei
“Nimejipanga kuhakikisha wananchi wa Himo wanapata maendeleo kama inavyosema ilani ya Chama cha Mapinduizi.Nitashirikiana na Serikali kila nyanja ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na kunufaika na rasilimali zao.” Kimei
MWANRI AMUACHA HOI PINDA “TUNAZAMA WOTE, TUNAPIGA MIAYO WANAOKATAA HABARI HII SUKUMA NDANI”