Kampuni ya GSM ambayo ni sehemu ya Wadhamini wa Yanga SC leo wametangaza kubadili mfumo wa utoaji wa bonus za wachezaji hao katika ushindi wa mechi.
GSM kupitia kwa Mkurugenzi wake wa uwekezaji Eng. Hersi Said ameyaeleza hayo leo mapema katika mahojiano na Azam TV na kusema sasa watakuwa wanagawa idadi ya mechi katika utoaji wa bonus na sio mechi moja moja kama ilivyokuwa msimu uliopita.
”Mwaka uliopita tulikuwa na bonus ya kila mechi kwamba mechi hii mkishinda mnapata hivi mkidroo hampati kitu, mkifungwa hampati kitu lakini kuna methodology nyingine ya kufanikiwa kitu fulani kwa mfano katika point 15 tunatakiwa kupata point 10 au tukipata point 15 bonus ni hii” – Hersi Said
”Tukipata point 10 hela inapungua kidogo tukipata point 5 nje ya point 15 tulizokuwa tunawania hauna sababu ya kupata chochote” Hersi Said
Msimu uliopita GSM ambao ni wasambazaji wa jezi za Yanga SC walikuwa wakitoa bonus ya Tsh milioni 10 katika kila mechi Yanga wanaopata ushindi Ligi Kuu kasoro game dhidi ya watani zao wa jadi Simba, round ya kwanza waliahidiwa Tsh milioni 50 ya pili ilikuwa Tsh milioni 200.