Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Bonde la Rufiji (RUBADA), Aloyce Masanja, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 14 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kosa la wizi wa Sh.Mil 86.
Masanja pia ametakiwa kulipa fidia ya Sh.Mil 86 kwa kampuni mbili za kilimo zilizoingiza fedha kwa mshitakiwa huyo.
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando ambapo amesema, mahakama imeridhika na ushahidi wa mashahidi watano wa upande wa mashtaka ambao wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa ni kweli mshtakiwa ametenda kosa.
“Baada ya kupitia ushahidi wote mahakama imebaini kuwa upande wa mashtaka umethibitisha mashitaka haya bila kuacha shaka kwamba mshitakiwa aliibia fedha za Rubada, hivyo umetiwa hatiani kwa mashtaka yote na kila kosa utatumikia kifungo cha miaka 14 gerezani lakini adhabu itakwenda sambamba na utatakiwa kulipa fidia ya Sh.Mil 86 na endapo ukishindwa, upande wa mashtaka utatakiwa kuuza mali za mshitakiwa ili walipwe,” Augustina Mmbando