Mgombea wa Urais Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema akichaguliwa, atahakikisha wakulima wa viungo na karafuu wanakuwa huru kuuza mazao yao sehemu yoyote wanayotaka duniani.
Kazi ya Serikali yake itakuwa ni kukusanya kodi ndogo ili kuwafanya wakulima wapate faida kubwa ili waweze kuendeleza kazi yao.
Amesema, Serikali ya CCM imekuwa ikichukua faida kubwa kuliko wakulima wenyewe lakini Serikali yake itawapatia Wakulima mbinu na mazingira bora ili wachangie kukuza uchumi wa Zanzibar.
Ameongeza kuwa, utawala wake utawashauri wakulima wa bidhaa za viungo kujikita zaidi kwenye viungo ambavyo vitaleta tija za haraka kwao na Serikali kwa ujumla.