Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amekemea vitendo vya wanaodaiwa kuwa wapambe wa baadhi ya wagombea kutekwa, kuteswa, kuumizwa na kutupwa pembezoni mwa mito, mifereji, misitu na barabara, matukio hayo yametokea Majimbo ya Hai, Vunjo, Rombo na Moshi Vijijini
Watuhumiwa zaidi ya 4 wamekamatwa wakidaiwa kuwanywesha pombe wapambe ili kupata taarifa za siri kuhusu mikakati ya kushinda nafasi za Udiwani na Ubunge.
“Kama Mkoa hatutakubali kuona vitendo viovu vinaendelea, na jambo hili kwa namna moja au nyingine litakwamisha wagombea wa vyama tofauti kutoa sera zao lakini pia wananchi watashindwa kwenda kuwasikiliza” RC Mghwira
Amewaagiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wagombea wa nafasi mbalimbali kutoka vyama vyote wanakuwa na ulinzi wa kutosha ili kuepuka vurugu.