Mamlaka nchini Urusi zimemkamata Polisi mstaafu wa kikosi cha usalama barabarani anayedai kuwa yeye ni ‘Yesu’ aliyezaliwa upya na kuendesha shughuli za ibada katika eneo la Siberia kwa miongo mitatu iliyopita.
Polisi wakiwa na helikopta na silaha walivamia jamii zinazoendeshwa na mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Sergei Torop, anayejulikana kwa wafuasi wake kama Vissarion na kumkamata yeye pamoja na wasaidizi wake wawili.
Bwana huyo na wenzake wameshtakiwa kwa kuanzisha kundi haramu la kidini, ambalo ibada zake zimehusishwa na kukusanya pesa kutoka kwa waumini na kuwafanyia unyanyasaji.
Polisi walimuonyesha mtu huyo mwenye umri wa miaka 59 akionekana kuwa na nywele ndefu na ndevu, sawa na yule anayeonekana kwenye picha kama Yesu.
ZITTO KABWE ATOA TAMKO RASMI SAKATA LA MGOMBEA URAIS TUNDU LISSU NA MEMBE