Leo September 24, 2020 Serikali ya Botswana inakusudia kuanzisha matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Shule za Msingi, Waziri wa Elimu ya Msingi, Fidelis Molao amesema matumizi ya lugha ya Kiswahili yataanzishwa katika Shule ndani ya siku zijazo.
Kiswahili ni lugha ya Kibantu inayozungumzwa sana katika eneo la Maziwa Makuu na sehemu zingine za Mashariki na Kusini Mashariki mwa Afrika ikiwa ni pamoja na Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na sehemu za Malawi.
Kiswahili kikitumika Botswana itakuwa ni lugha ya kwanza ya Kiafrika kutumika kutoka nje ya mipaka ya nchi hiyo ambayo ni mzalishaji mkubwa wa Almasi Ulimwenguni.
Molao amesema Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) itakuwa na Washirika wakubwa wa kibiashara na nchi nyingi zinazozungumza Kiswahili katika siku za usoni jambo ambalo hata Botswana inalihitaji zaidi katika kukuza uchumi na mauzo ya nje.