Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kuwa wameamua kujitegemea wenyewe kwenye mambo ya msingi badala ya kutegemea mikopo.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa Terminal III ya Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Kisauni amesema mradi huo umelipiwa na fedha za ndani na hawajakopa pahala popote.
“Kwahiyo sasa ndugu wananchi tumeamaua tunajitegemea wenyewe kwenye mambo ya msingi lazima tufanye wenyewe hii kukopakopa wakati mwingine tunachelewesha maana mpaka wakubali wenyewe ndo watukopeshe” Dkt.Shein
“Lakini tukipanga vizuri bajeti yetu wenyewe tutafanya mambo mengi sana, tumeonyesha njia miaka miwili iliyopita” Dkt.Shein
MASHABIKI WA YANGA WALIOFANYIA FUJO MASHABIKI WA SIMBA WANATAFUTWA NA POLISI