Umoja wa Mataifa unaadhimisha siku ya kimataifa ya kufasiri, kwa kutambua umuhimu wa kufasiri kwa lugha kama kitu kinachoyaleta mataifa pamoja kupitia mijadala, uelewa na mahojiano.
Kuonyesha hilo Umoja wa Mataifa umeandika kuwa, hadi sasa wana lugha sita rasmi zinazotumika na Umoja wa Mataifa ambazo ni Kiarabu, Kichina, Kiingereza, Kifaransa, Kirusi na Kihispania.
Watendaji huongea lugha yoyote ambayo hufasiriwa kwenye lugha rasmi za UN. Huku wakisema kila taarifa ya UN hupitiwa na mhariri kabla ya kufasiriwa.
Katika suala la ufasiri Tamko la Haki za Binadamu Duniani (Universal Declaration of Human Rights) linashikilia rekodi ya Guinness ya kuwa nyaraka iliyotafsiriwa zaidi, ikiwa imetafsiriwa katika zaidi ya Lugha 500.
DUUH! NDOA IMEVUNJIKIA HONEYMOON, BIBI HARUSI ALIALIKA MCHEPUKO WAKE HARUSINI