Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na familia ya kijana Briton Wilfred Mollel (26) aliyeuawa kikatili tarehe 25 Agosti, 2020 baada ya kushambuliwa katika vurugu zilizotokea wakati wa urejeshaji wa fomu za kugombea udiwani kwa msimamizi wa uchaguzi wa Kata ya Kaloleni katika Jimbo la Tunduma Mkoani Songwe.
Rais Magufuli amekutana na Mama wa Marehemu aitwaye Roda Bryson Mwaisongole na Mjane wa Marehemu aitwaye Salome Philemon Mayao Mjini Tunduma ambapo amewapa pole na kutoa ubani wa shilingi Milioni 6.