Oktoba 4 , 2020 Mbungea aliyepita bila kupingwa Jimbo la Ludewa kupitia CCM Wakili Msomi Joseph Kamonga ameendelea na Kampeni zake katika kata za Manda , Iwela na Luhuhu jimboni humo kwa lengo la kuwaeleza wananchi nini atawafanyia katika kipindi cha utawala wake , kupokea changamoto za kata husika pamoja na kuwanadi viongozi wengine kupitia chama chake wakiwemo Madiwani pamoja na Rais.
Akiongeza na Wananchi wa Vijiji vya Kata hizo wakili kamonga amesema ” Ndugu zangu mimi ni Mtoto wenu nimesoma manda sekondari kwahiyo Changamoto za Manda nazijua , nimebeba sana Madumu ya Maji kutoka Ziwani hapa kupeleka Shuleni Manda Sekondari hivyo changamoto za Manda Sekondari na hapa sijasimuliwa ila nazifahamu mwenyewe kwahiyo mimi ni mwenzenu “. – Wakili Joseph Kamonga
”Ninawashukuru sana wana Ludewa wote kwa imani kubwa mliyoionyesha kwa Chama cha Mapinduzi na Rais wetu mpendwa Dr John Pombe Magufuli mbaka mkaona ni vyema Mbunge wenu wa Ludewa apite bila kupingwa , kwangu mimi naona nina deni kubwa sana la kuwatumikia wana Ludewa sawasawa na imani ambayo mmeionyesha kwa hiyo nawahakikishia Ndugu zangu nitawatumikia kwa Utumishi uliotukuka nitatumia Karama zangu zote alizonipa mwenyezi Mungu kuhakikisha yale ambayo yamo katika ilani ya Chama cha Mapinduzi yanatekelezwa , lakini pia nitakuwa nakaa Nanyi ndugu zangu ili niweze kujua vipaumbele vyenu ni vipi ili mambo yaweze kuwa Mazuri.- Wakili Joseph Kamonga
Akizungumzia changamoto ya Maji katika kata hizo amesema kuwa tayari hatua za muda mfupi zimeanza kuchukuliwa ili Wananchi waweze kupata Maji safi na Salama ikiwemo uchimbaji wa Visima na tayari kisima kimoja kimeshachimbwa katika Kata ya Sagalu lakini pia ataishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kutumia Maji ya Ziwa Nyasa kutatua changamoto hii ya Maji.
”Lakini kuna hoja ya Maji wale waliokuwepo wakati tunampokea Mama Samia nilizungumzia suala hilo naamini mlisikia , niliomba kama ziwa Viktoria wameweza kutumia Maji yale kutatatua Changamoto ya Maji hadi Mikoa ya jirani basi nasisi tufikilie Wizara itume Wataalamu waje waona uwezekano wa kutumia Maji haya kwaajili ya kutatua changamoto hii katika kata za Nsungu , Ruhuhu na Tarafa nzima ya Masasi kwahiyo hoja hii ilipokelewa na Makamu wa Rais na tutarajie itafanyiwa Kazi, lakini kuna zaidi ya milioni miatatu zimetoleka na kuna Wataalamu wanafuatilia Maji yanayotoka Lifua kuja Manda kwahiyo tutakuwa na mipango ya muda mfupi ambayo ni uchimbaji wa Visima na mipango ya muda mrefu ili kutatua tatizo hili ”.- Wakili Joseph Kamonga