Derek Chauvin, Askari wa Minneapolis ambaye alishtakiwa kwa kosa la kumuua Mmarekani mweusi George Floyd yupo nje baada ya kuachiwa kwa dhamana yenye thamani ya USD Milioni moja, hukumu yake inatarajiwa kutolewa Mwezi March mwakani baada ya Mahakama kumkuta na hatia ya mauaji.
Askari huyo amekuwa Gerezani tangu May 31 baada ya video yake kusambaa akimkanyaga George Floyd shingoni hadi akakosa pumzi na kufariki Dunia, tukio ambalo liliibua maandamano makubwa Marekani na Mataifa mengine Duniani.
Derek, amepewa masharti ya kuhudhuria Mahakamani kila atakapohitajika bila kukosa, kutomiliki silaha, kutofanya kazi yoyote ya ulinzi na usalama ikiwemo upolisi na pia hapaswi kuwasiliana na Ndugu yoyote wa George iwe ni uso kwa uso au mitandaoni.