Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge, abadilike na kuachana na upole badala yake awe mkali kwa lengo la kuhakikisha miradi ya jiji hilo inaenda vizuri.
“Wahandisi wa mikoa na wilaya hamieni hapa msimamie huu mradi kwa hiyo uongozi wa mkoa, ninajua mkuu wa mkoa wewe ni mgeni hapa lakini badilika uwe mkali usiwe sheikh au Askofu, ni lazima watu watimize wajibu wao, muondoa ‘damage’ ambayo iko kwenye mkataba” Rais Magufuli