October 9, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Dkt. Athuman kihamia kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na Maofisa wa Mamlaka ya Mapato TRA wamefanikiwa kukamata simu bandia za magendo zenye thamani ya Milioni 700.
Akizungumza katika boda ya Tarakea yalipokamatiwa magendo hayo ikiwemo simu janja za gharama, Kihamia amesema kwamba mzigo huo wa bidhaa hiyo uliingia nchini kwa njia za panya ambapo ulichanganywa na mzigo wa ndizi ukisafirishwa kuelekea Mkoa ni DSM.