Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Dodoma imemuhukumu Tibu Madeha na Abdallah Mbwana kwenda jela miaka ishirini baada ya kukutwa na hatia ya kupatikana na nyara za Serikali (vipande 9 vya ngozi za chui) vyenye thamani ya Tsh 31,122,000/= na kufanya biashara ya nyara bila vibali.
Katika kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi Na. 3/2018 ilivyokuwa mbele ya Lushasi, Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ukiongozwa na Mawakili wa Serikali Judith Mwakyusa na Harry Mbogoro.
Aidha mahakama hiyo pia imetaifisha nyara hizo na kuwaachia huru washtakiwa wengine wawili ambao ushahidi dhidi yao haukuwagusa.